Monday 6 June 2016

Haya ndio maneno ya Zitto Kabwe yanayomlenga Rais Magufuli kuhusu Naibu Spika wa Bunge.

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala jana alisema Naibu Spika wa Bunge , Tulia Ackson ambaye kwa sasa anapigwa na wabunge wa upinzani


kwa kutokuwa na imani naye kutokana na uendeshaji wake wa shughuli za bunge. Zitto Kabwe amedai Naibu huyo ameletwa bungeni hapo kutoka Ikulu na walimleta bungeni ili awe Spika wa Bunge jambo ambalo liligonga mwamba.

Mbali na hilo Zitto Kabwe alisema kuwa Rais wa nchi, John Pombe Magufuli ndiye aliyepanga viongozi wa bunge na kumleta Naibu huyo ili waweze kulipeleka bunge vile wao wanavyotaka.

"Na nyinyi wananchi mnajua kuwa Naibu Spika wa Bunge ametoka Ikulu, Kwanza walimtaka awe Spika wa Bunge lakini baada ya wabunge kuweka ngumu wakasema basi awe Naibu Spika sababu wanajua kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ni mgonjwa mara kwa mara anakwenda kwenye matibabu. Kwa hiyo watamtumia mtu wao kupeleka bunge vile wao wanavyotaka na ndiyo maana mnamuona muda mwingi yupo yeye tu" alisema Zitto Kabwe.


zUSISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment