Monday, 6 June 2016

Hii ndio Kauli ya mwisho ya serikali kuhusu mpango wa kuzima simu feki nchini.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani


Serikali imesema kuwa lengo kuu la kutekeleza zoezi la kuzizima simu feki nchini Tanzania ni pamoja na kudhibiti matukio ya uhalifu yanayofanyika na simu  ambapo serikali inashindwa kuzifauatilia kwa kuwa hazina vigezo vya kusajiliwa.


Hayo yamezungumzwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani na kuongeza kuwa ili sheria ya mtandao iweze kufanya kazi kwa ukamilifu ni kuhakikisha simu zote zinazotumiwa na Watanzania zinakuwa zimesajiliwa.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa polisi wanashindwa kufuatilia kesi nyingi za makosa ya mtandao ambazo watu wanakwenda kuripoti kutokana na tatizo hilo la simu feki huku akisisitiza kuwa tarehe 16 mwezi huu saa sita usiku ndio itakua mwisho wa simu hizo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ngonyani amesema kuwa tangu kuanza kwa sheria hiyo hakujaripotiwa kesi kuhusu matumizi mabaya ya mtandao lakini kabla ya kuanza kwa sheria hiyo kuliripotiwa matukio 59 huku akiongeza serikali haifatilii kila mtu isipokuwa pale mtu anapoenda kutoa taarifa ya tukio.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment