Wednesday, 8 June 2016

Hizi ndio sentensi Tano alizoeleza Zitto Kabwe baada ya kuojiwa na jeshi la polisi hii leo.

 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefika Makao makuu kanda maalum ya Dar es salaam, ikiwa ameitikia wito wa polisi.


 Zitto amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.
 Zitto Ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.

Amesema, Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya demokrasia.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.

“Mambo kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.

“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.

Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.

Jeshi hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba, wanasheria wa ACT-Wazalendo  wataenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi.

“Lakini kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.

“Lazima tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.

“Kimsingi nimehojiwa
1) maombi yetu ya mkutano ilikuwa ‘kujenga chama’ lakini Sisi tulizindua operesheni linda demokrasia

2) kusema Rais ameropoka kuhusu sakata la sukari

3) kumchonganisha Rais na wananchi kuhusu suala la vilaza

4) kumgombanisha Rais na wananchi kwa kusema yeye anajifanya Rais wa masikini na hivyo kumgombanisha na wasio masikini

5) kumwita Rais dikteta na kwamba anaendesha nchi kwa imla. Yote hayo chini ya kufungu 89(1)(a) cha Penal Code ” kutumia maneno ya matusi yenye kuweza kuvunja Amani ( abusive language )”


Steven Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.

“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.

“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”

Jeshi la Polisi limemuomba Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi. 


USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment