Wednesday 1 June 2016

Jaji Mkuu chande azungumza haya kuhusu ukubwa wa tatizo la Rushwa katika Mahakamani.

Mhe. Jaji Mkuu ameyasema hayo mjini Musoma mkoani Mara, wakati akizungumza na watumishi wa idara ya mahakama za mkoa wa mara, ambapo amesema tafiti hizo ambazo zimefanywa na idara
ya mahakama yenyewe kupitia taasisi hizo, zimebaini rushwa na vitendo vya utendaji mbovu kwa baadhi ya watumishi wa idara ya mahakama vimelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi.

Hata hivyo Jaji mkuu amemweleza mkuu wa mkoa wa Mara, kuhusu mipango ya ujenzi wa mahakama kuu mkoani mara, hatua ambayo amesema mbali na kuwapunguzi kero wananchi pia itarahisha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Katika ziara hiyo Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Othman Chande, pamoja na kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali na idara ya mahakama, pia amepata fursa ya kutembelea mahakama za mwanzo, wilaya na mkoa pia eneo linalotarajia kujengwa mahakama kuu mkoani mara.

No comments:

Post a Comment