Wednesday 1 June 2016

Jeshi la polisi visiwani zanzibar wazungumza haya baada ya kumuhoji Maalim Seif.

kamishina wa jeshi la polisi Zanzibar Omar makame

Naibu Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai visiwani Zanzibar Bw. Salum Msangi amesema kuwa kuhojiwa kwa kiongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Hamad hakuna shinikizo toka mahali popote.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Visiwani humo Bw. Msangi amesema zoezi la kuhojiwa kwa Maalim Seif si pekee bali wataendela kufanya hivyo kwa yoyote mweye kutoa kauli ambazo zinaviashairia vya uvunjifu wa amani.

Ingawa hakueleza kwa kina undani wa mahojiano hayo na kiongozi huyo, Msangi amesema wameshamaliza kumhoji na ameachiwa kwa dhamana ya watu wawili wakati wakiwa wanaendela na uchunguzi wao juu ya matukio yanayojiri visiwani humo.

Kwa upande wake Msemaje wa Chama cha CUF, Salim Bimani ameonyeshwa kusikitishwa kwake na jeshi la Polisi Zanzibar kumhoji kiongozi huyo huku akilituhumu jeshi hilo kwa makatazo wanayoyafanya juu ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment