Masauni ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula aliyetaka kujua ahadi ya serikali ya kujenga nyumba za polisi jiji la Mwanza ndani ya wiki 36 ambapo nyumba hizo hazikukamilika na kuleta usumbufu mkubwa wa makazi kwa askari polisi.
‘’Tumetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huu na serikali itakamilisha na miradi mingine ya nyumba za polisi zenye uwezo wa kubeba familia 12’’ Amesema Naibu Waziri Masauni.
Aidha Naibu Waziri amesema kukamilishwa kwa nyumba hizo kutaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za polisi katika mikoa 17 kama serikali ilivyoahidi ili kusaidia kutatua kero ya muda mrefu ya makazi ya polisi.
No comments:
Post a Comment