Tuesday, 7 June 2016

Tanzania kuanza kusafisha mbegu za kiume zilizona virusi vya ukimwi.

Wanaume wanaoishi na virusi vya Ukimwi sasa huenda wakapata suluhisho la kupata watoto na wenza wao ambao hawana virusi hivyo, baada ya kuwapo tiba ya kusafisha mbegu za kiume zenye VVU hapa nchini.

Tiba hiyo sasa inapatikana hapa nchini katika hospitali moja iliyo jijini Dar es Salaam, ambayo inatoa huduma za uzazi na upandikizaji wa mimba katika mirija ya uzazi kitaalamu inayojulikana, In Vitro Fertilization,(IVF). Kwa sasa, njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (MTCPT) ndiyo inayotumika duniani kote kwa mjamzito kupewa dawa za ARV wakati wa ujauzito zinazokinga maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na baada ya mtoto kuzaliwa.

Kadhalika mtoto hutakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita au kutonyonya kabisa ili asipate maambukizi.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment