Thursday 2 June 2016

Waangalizi wa uchaguzi watoa ripoti yao kamili kuhusu uchaguzi wa Oktoba 2015


Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania umewasilisha ripoti yake kamili kuhusu
uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana iliyo na mapendekezo kadhaa ya marekebisho, lengo likiwa kuboresha mchakato wa uchaguzi ili kuongeza imani ya wananchi kuhusu chaguzi zijazo.

Akiwasilisha ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini dar es salaam mwangalizi mkuu wa ujumbe huo wa EU Bi Judith Sargentini amesema ripoti hiyo iliyoshirikisha chaguzi zote mbili Tanzania Bara na Viziwani imeainisha baadhi ya mapungufu yanayopaswa kuangaliwa kuhusu mfumo wa kiuchaguzi pamoja na mchakato wa uchaguzi kupitia tume ya taifa ya uchaguzi NEC na tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC huku taasisi za usimamizi wa uchaguzi zikishindwa kuonyesha uwazi kamili juu ya michakato yao ya kufanya maamuzi.

Kuhusu uchaguza wa Zanzibar, Bi Sergintini amesema kufuatia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, umoja wa Ulaya pamoja na waangalizi wengine wa Kimataifa wamezungumzia wasiwasi wao na kuiomba ZEC iwasilishe ushahidi wa kuhalalisha uamuzi huo ambao hata hivyo haukuwasilishwa na kuwafanya waangalizi hao kutoshiriki uchaguzi wa marudio kutokana na mazingira ambayo hayakuonyesha uchaguzi shirikishi, halisi na wa kuaminika.

Mapendekezo yaliyo ndani ya ripoti hiyo ambayo baadhi yaliwasilishwa mwaka 2010 ni pamoja na haki ya wagombea binafsi, kuruhusu haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kisheria, haki ya vyama vya siasa kuunda umoja wa kiuchaguzi, kuangalia upya shria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015, kuendelezwa kwa muundo wa kudumu wa NEC katika ngazi za mikoa na marekebisho ya ,chakato wa uteuzi wa makamishna wa uchaguzi wa NEC na ZEC

USISAHAU KULIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA,KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment