Monday 6 June 2016

Yatazame haya maajabu ya Wanasayansi wa marekani kukuza viungo vya binadamu kwa kutumia Teknolojia hii.


Wanasayansi nchini Marekani wanajaribu kukuza viungo vya binadamu ndani ya mwili wa nguruwe, wakitumia teknolojia mpya inayofahamika kama 'Gene Editing'.


Image copyright
Image captionWanasayansi kukuza viungo vya binadamu ndani ya nguruwe
Wanasayansi hao wametoa vinasaba vinavyosaidia ukuaji wa kongosho kwenye nguruwe na badala yake wanaweka chembe chembe za viungo vya binadamu kwa matarajio kuwa kongosho ya binadamu itakua.
Image copyright
Image captionHata hivyo teknolojia hiyo mpya inapingwa vikali na wanasayansi wengine kwa sababu ya maadili ya udaktari.
Wataalamu katika chuo kikuu cha California, Davis wanaamini kuwa utafiti huo utasaidia kupunguza uhaba wa viungo vya binadamu.
Hata hivyo teknolojia hiyo mpya inapingwa vikali na wanasayansi wengine kwa sababu ya maadili ya udaktari.
Wanasayansi hao wanadai kuwa huenda chembe chembe za binadamu zitakuwa na kufika kwenye ubongo wa nguruwe unaoendelea kukuwa.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment