Leo Jumamosi, July 23, 2016 ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi(CCM) kumthibitisha Rais John Magufuli ili awe mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi kumpokea kijiti mwenyekiti anayeng'atuka, Rais mstaafu, Dokta Jakaya Kikwete.
Kikwete: Nimeambiwa hali ya usalama ni nzuri na ya uhakika. Tumealika watu mbali mbali ikiwemo mabalozi na viongozi wa vyama vya siasa, kuja kwao ni jambo la heshma na tunawaomba muendelee ushirikiano na chama chetu kitarudisha maradufu upendo mliotuonyesha kwetu.
Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1990, Mwl Nyerere alipong'atuka na kumuachia mzee Mwinyi, mara ya pili ilikuwa Juni 1996 alipong'atuka mwenyekiti Mwinyi na kumuachia Mkapa na Juni 2006 nilikabidhiwa, leo zamu yangu.
Tulifanya kazi ya ziada kumshawishi Rais Magufuli awe mwenyekiti wa chama, nilipomwambia mara ya kwanza mwezi February aliniambia yeye hana haraka na mimi niendelee. Nadhani kunifanya niachane na hayo mazungumzo, akanikaribisha ugali na baada ya kula tukaagana.
Urais ni ofisi kubwa sana, siku hizi mimi nalala, usingizi unaisha. Mzee usingizi hauishi. Majibu ya Rais Magufuli hayakunishangaza kwani hata mimi nilipoambiwa mara ya kwanza nilimkatalia mzee Mkapa lakini baadae mazungumzo yalifanyika.
Tofauti ya wakati ule na sasa, hakukuwepo vyombo vya habari na watu waongo na wafitini. Hakukuwepo na wakati wowote wa mimi kukataa, wakageuza eti mimi sitaki kutoka, wanataka wanihukumu mimi kwa uongo wao.
Safari yangu ilianza Aprili 1975 nilipowasili Singida kuwa katibu msaidizi wa TANU mkoa wa Singida na mwaka mmoja baadae nikapelekwa jeshini, nikaenda Zanzibar na kupawa dhamana ya kuandaa mfumo mpya upande wa Zanzibar, nilihuzika kuandaa mchakato wa kupata viongozi wa chama. 1980 nilihamishiwa ofisi ndogo ya makao makuu Dar es Salaam, 1981 nikaenda Tabora, 1983 nikarudishwa jeshini, miaka mitatu baadae nikahamishiwa Nachingwea. Mwaka 1988 nikamaliza kwenye chama na kuwa mbunge na kuteuliwa naibu waziri wa nishati na madini na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Natoa shukrani zangu za dhati kwa wazee wawili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, yeye ndie aliyenifanya nijulikane kwa watanzania. Wa pili ni mzee Benjamin Mkapa, namshukuru kwa kuniamini na kunipa dhamana ya kuongoza diplomasia Tanzania kwa miaka kumi mfululizo, iliniwezesha kuijua dunia na watu mbalimbali duniani na ilinisaidia sana katika uongozi wangu nilipokuwa Rais.
Sina kitu wala namna ya kuwalipa mzee Mwinyi na mzee Mkapa kwa waliyonitendea maishani, nawaombea maisha marefu.
Mheshimiwa Kikwete kamaliza kutoa hotuba yake ya kuaga na kumaliza kwa kumshukuru mke wake, mama Salma Kikwete na kumshukuru kwa kuwa ana mchango katika kipindi chote cha mafanikio yake pia amewashukuru wanawe na wajukuu zake kwa kumkosa baba na babu yao pia kwa kuwa wahanga mara kadhaa kutokana yeye kuwa mwanasiasa.
Mzee Yusuph Makamba.
- Kikwete anachukia ufisadi kiasi cha kumkata rafiki yake kipenzi, Lowassa.
- Askofu Gwajima alisema uongo, kisha anamsingizia Jakaya kuwa amekataa kumuachia Magufuli.
- Pengo la jino la dhahabu Jakaya Kikwete linazibwa na jino lingine la dhahabu Magufuli.
- Kocha anaondoka lakini hatuachi peke yetu, anatuachia kocha alietupa ushindi uchaguzi ulioupita.
- Alichosema Magufuli, amekataa vimemo ikiwemo changu, kuna tofauti kati ya vimemo na ushauri na ushauri wangu ameukubali.
- Jakaya aliwabatiza kwa maji, Magufuli atawabatiza kwa moto.
MSIKILIZE Hapa Mzee Makamba
No comments:
Post a Comment