Sunday, 24 July 2016

Picha zote za Tukio zima la Mkutano mkuu wa CCM, Jackline Wolper kurudi CCM Rasmi Tazama

Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio zipatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika. 
Mwenyekiti Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kumi.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10,pichani katikati anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho 
Wake wa viongozi wakishangilia baada ya Mwenyekiti Mpya wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho 

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyakuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana Julai 23, mkoani Dodoma.
Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kimpya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipiti cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho.



USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment