Monday 18 July 2016

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ashangazwa na jambo hili kutoka CITD.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kushangazwa kwake na kitendo cha mfuko wa wakfu wakuendeleza zao la korosho nchini  CITDF kukaa na shilingi bilioni 37 kwenye akaunti yao huku wakishindwa kuendeleza zao hilo kwa kuwapa elimu wakulima jambo ambalo linachangia kushuka kwa uzalishaji wa zao la korosho nchini.

Mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la korosho Moja ya majukumu ya mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la korosho ni kusimamia uendelezaji wa zao hilo kwa kutoa mbegu mpya sambamba na elimu ya utunzaji wa mikorosho.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watendaji wa wilaya za mkoa wa Mtwara,amesema uzalishaji wa zao la korosho unashuka kutokana na wakulima kuendelea na kilimo cha mikorosho ya zamani ambayo haizai kwa wingi huku mfuko wa wakfu wenye dhamana ya kuendeleza zao hilo hauchukui hatua zozote za kuwapa wakulima mbegu mpya.

Aidha waziri mkuu amesema ili kuhakikisha mkulima wa korosho ananufaika na mfumo wa stakabadhi ghalani viongozi wa serikali wanapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mnunuzi wa zao hilo anaweka bondi ya fedha benki kabla ya kupewa dhabuni ya kununua korosho.

No comments:

Post a Comment