Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amekanusha taarifa zilizotolewa katika mitamdao mbalimbali ya kijamii zikimuhusisha yeye kupinga agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam Paul Makonda la kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuwatambua watu wasio na kazi maalum.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Meya wa jiji la Dar es salaam amsema kuwa taarifa hizo zlizosambaa katika mitandao ya kijamii julai 15 mwaka huu ni za uazushi na zenye lengo la kumchafua sambamba na kuipotosha jamii hivyo wananchi kutakiwa kuzipuuza.
Aidha Meya wa Jiji Isaya Mwita amsema kuwa majukumu ya jiji ni kuratibu na kusimamia shughuli za uendelezaji wa jiji katika Halmashauri za manispaa zilizopo katika jiji la Dar es salaam pamoja na kushughulikia masuala mtambuka katika mamlaka za jiji hilo na si kupinga kazi ama agizo la Mkuu wa Mkoa kama ambavyo taarifa hizo za uzushi zilivyobainisha.
Bwana Isaya Mwita amewataka wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kuungana katika kuliletea maendeleo jiji hilo na si kutengeneza taarifa za Uzushi zisizo na tija kwa Taifa huku akiitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuwachukua kuwashughulikia watu wanaoneza uzushi kwenye mitandao ya simu na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment