Friday, 5 August 2016

Hiki ndio kiwango cha mapato kilichokusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' kwa Mwezi July.2016.

[​IMG]

Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' imekusanya zaidi ya trilioni 1.055 sawa na 95% ya lengo kwa mwezi wa July 2016. Katika mwaka huu wa fedha TRA imepewa lengo la kukusanya trilioni 15.1 ikilinganishwa na lengo la trilioni 13.32 kwa mwaka ulioisha.



Pia imesema kuwa itaanza kuwabana wenye nyumba za kupanga ili waweze kulipa kodi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema watazunguka nyumba kwa nyumba kuhakikisha wapangaji wanatoa mikataba na inalipiwa kodi.




USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment