Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora Ulaya.
Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa Ulaya baada ya kuwashinda wachezaji wengine wawili ambao wote wanatokea katika timu za jiji la Madrid nchini Hispania tuzo hizo zilitolewa Nchini France katika mji wa Monaco.
Gareth Bale (kulia) ,Ronaldo na Antoine Griezmann upande wa kushoto. |
Katika Kura zilizopigwa na waandishi 55 wanachama wa UEFA katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2015/2016 matokeo yamekuwa hivi
Cristiano Ronaldo – 40
Antoine Griezmann – 8
Gareth Bale – 7
Mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya Norway Ada Hegerber ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa upande wa Wanawake 2015/2016
Ada Hegerberg.
No comments:
Post a Comment