Wednesday 31 August 2016

Taarifa kuhusu Mgogoro kati ya wenyeviti wa serikali ya Mitaa katika kata ya Vingunguti na Afisa mtendaji.

Image result for news
Mgogoro Mkubwa Umeibuka kati ya wenyeviti wa serikali ya Mitaa katika kata ya Vingunguti na Afisa mtendaji wa kata hiyo ambapo majira ya asbhi wenyeviti hao wakiongozwa na diwani wao walizifunga kwa minyororo na kufuri ofisi za afisa mtendaji kata kwa tuhuma lukuki zikiwemo madai ya ubadhilifu.

wenyeviti  wamedai kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kutokuwa na Ushirikiano wa kiutendaji pamoja na mtendaji kata ambapo pia walionyesha barua ya uhamisho iliyotolewa na mkurugenzi wa manispaa ya ilala ya August 10 ya uhamisho wa afisa mtendaji kata lakini wakadai bado anaingia katika ofisi hizo zilizopo buguruni mtaa wa mtambani.
Afisa Mtendaji anayetuhumiwa Bw,San Swila  amekiri kuwepo kwa mgogoro ambao amedai kuwa unatokana na tofautia za kiitikadi,lakini pia alikanusha madai ya ubadhilifu dhidi yake huku pia akisema hana taarifa ya uhamisho kwa kuwa hajapatiwa barua rasmi na ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ilala.
USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment