Thursday 15 September 2016

Edward Lowasa azungumza haya kuhusu udikteta wa serikali ya Rais Magufuli.

Image result for edward lowassa
Aliyekuwa mgombea wa uraisi Edward Lowassa amemkosoa  rais John Magufuli kwa kile alichokitaja kuwa ''chembechembe za kidikteta'' katika serikali yake.

Akizungumza na mwandishi wa BBC John Nene nchini Kenya, amesema kuwa alitaraji kwamba rais Magufuli angeondoa urasimu serikalini lakini "kuna mambo mengine hayajakwenda sawa ", ijapokuwa alikataa kutoa mifano alipotakiwa kufanya hivyo.
Bwana Lowassa alikuwa katika chama tawala alipokuwa waziri mkuu, lakini mwaka uliopita alijiunga na upinzani wa CHADEMA ambapo alishindwa na Rais Magufuli wakati wa uchaguzi.
Magufuli aliyepewa jina Tinga (Bulldozer) anajulikana kufanya maamuzi yanayopendwa tangu achukue mamlaka mwaka uliopita, kama vile kufutilia mbali sherehe za uhuru wa taifa hilo ili kuhifadhi fedha.
Lakini wakosoaji wake wamemshtumu kwa kukabiliana vikali na wapinzani.
Gazeti moja linalodaiwa kuwa mkosoaji mkubwa wa uongozi wake hivi majuzi lilifungwa huku mtu mmoja akikamatwa kwa madai ya kumtusi katika mitandao ya kijamii.

Rais John Magufuli
Serikali yake pia imepiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja ile ya faraghani ya kisiasa.
Maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanywa dhidi ya serikali yaliahirishwa mwezi huu baada ya viongozi wa kidini kujitolea kuongoza mazungumzo na serikali.
Bwana Lowassa amesema kuwa maandamano yalilenga kupinga ''chembechembe za udikteta katika serikali'.
Aliambia wanahabari kwamba ana matumaini kuhusu mazungumzo hayo lakini hatosema kile upinzani utakachofanya iwapo yatafeli.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment