Wednesday 14 September 2016

Hii ndio kauli ya Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Pro.Benno Ndulu kuhusu hali ya uchumi nchini.


Image result for Prof. Benno Ndulu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu, amekanusha kuwepo kwa mdororo wa uchumi nchini, na kusema kuwa uchumi wa nchi kwa sasa bado upo imara na unaendelea kukuwa kama ilivyotarajiwa.


Prof. Ndulu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia hali ya uchumi nchini na kwamba kinachoonekna sasa ni fedha kuhama kutoka katika mikono haramu kwenda kwenye matumizi halali na sahihi kwa uchumi.

Aidha, Profesa Ndulu amesema serikali haina mpango wowote wa kuchapisha noti mpya kwa sababu uchumi wa nchi ni imara na hakuna sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa sasa.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment