Thursday 1 September 2016

Hii ndio kauli ya Rais Magufuli kwa wale walioficha fedha,agusia kubadili NOTI.

Image result for Rais magufuli leo
Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.


Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.

Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment