Tuesday 6 September 2016

Hii ndio Miswada mitano iliosainiwa na Rais Magufuli kuwa Sheria.

Image result for Rais magufuli asain
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia na kusaini miswada mitano iliyojadiliwa katika mkutano wa tatu wa bunge kuwa sheria kamili za nchi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, wakati wa ufunguzi wa bunge la 11 Mkutano wa nne kikao cha kwanza kilichoanza leo mkoani Dodoma.
Mhe. Ndugai aliitaja miswada hiyo iliyotiwa saini na kuwa sheria ni pamoja na Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi wa Umma namba 5 ya mwaka 2016.

Pia Mhe. Ndugai amempongeza Naibu Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson na viongozi wengine waandamizi wa bunge hilo kwa kuweza kuliongoza kwa takribani siku 70 na kufanikisha kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Aidha Mhe. Ndugai ametumia fursa hiyo kuwaasa wabunge wa bunge hilo kusoma kila kinachowasilishwa bungeni kwa umakini na kuweza kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment