Ripoti ambayo imezinduliwa leo 29.09.2016 Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na chuo cha IFM), imebainisha maoni ya wananchi.
Maswali yaliyo ulizwa kwa wananchi
- Je, wananchi wana maoni gani kuhusu Rais Magufuli kuitwa dikteta?
- Je, wana lipi la kusema kuhusu Vyama vingi na uhuru wa kutoa maoni?
- Wanasapoti maandamano ya UKUTA, na wanapanga kushiriki?
Kwa mujibu wa ripoti hiyo imebainisha yafuatayo kwa takwimu kuhusu maswali hayo;
Takwimu: Asilimia 60 ya wananchi wanaunga mkono kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa, ikiwemo 31% ya wafuasi wa vyama vya upinzani.
Takwimu: Kuhusu utayari wa watu kujiunga na maandamano
Takwimu: 16% ya wananchi wanafahamu harakati za UKUTA, huku 79% wakiwa hawafahamu harakati hizo.
Takwimu: Miongoni mwa wale wanaofahamu UKUTA, 48% wameelezea kwa usahihi kuwa ni Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania.
Takwimu: Miongoni mwa waliokuwa wakifahamu harakati ya UKUTA, 9% kati yao walipanga kushiriki maandamano ya Septemba 1.
Takwimu: 69% ya wananchi wanaelezea demokrasia kama mfumo unaokubalika zaidi kuliko aina nyingine za mifumo ya serikali.
Takwimu: 80% ya wananchi wanasema kwamba baada ya uchaguzi, juhudi za kimaendeleo zipewe kipaumbele na vyama vya siasa.
Aidha 86% ya wananchi wanasema Tanzania inahitaji vyama vya upinzani ili wananchi waweze kuchagua vema nani wa kuwaongoza.
Pia 51% wanasema mikutano husaidia kuiwajibisha serikali na huchangia maendeleo, 49% wanasema huvuruga umakini wa serikali na wananchi.
Takwimu: 95%, wakiwemo wafuasi wa chama tawala na vyama vya upinzani wanaunga mkono haki ya wananchi kuikosoa serikali.
Takwimu: 48% ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaamini wanaweza kuikosoa serikali iliyopo madarakani (bila hofu), kuliko serikali iliyopita.
Takwimu: 71% ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanataka viruhusiwe kufanya mikutano na maandamano kama wanavyopenda, na si wakati wa kampeni tu.
Takwimu: 47% ya wananchi wanataka vyama vya upinzani viruhusiwe kufanya mikutano na maandamano kama wanavyopenda, na si wakati wa kampeni tu.
Takwimu: 15% wanalitafsiri neno udikteta kama mtu mmoja ndiye mwenye maamuzi nchini, 6% wamelitafsiri kama ubaguzi.
Takwimu: 26% ya wahitimu wa Vyuo, 13% ya wale wa sekondari, 10% ya wale wa msingi na 4% ya wasio na elimu wanaamini nchi inaongozwa na dikteta.
Takwimu: 13% ya wanaume wanamuita Rais dikteta huku 8% ya wanawake wakimuita hivyo.
Takwimu: 11% wanaamini Tanzania inaongozwa na dikteta huku 58% wakipinga, 31% wamesema hawajui.
Takwimu: 95%, wakiwemo wafuasi wa chama tawala na vyama vya upinzani wanaunga mkono haki ya wananchi kuikosoa serikali.
Takwimu: Mwananchi 1 kati ya 3 alitoa maana ya neno “udikteta” akilitafsiri kama kutawala kimambavu.
Takwimu: 15% wanalitafsiri neno udikteta kama mtu mmoja ndiye mwenye maamuzi nchini, 6% wamelitafsiri kama ubaguzi.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment