Wednesday, 12 October 2016

Marekani kuwapeleka binadamu katika sayari ya Mars kufikia miaka ya 2030.

Image result for mars planet
Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali ya taifa hilo itashirikiana na kampuni za kibinafsi katika mpango ambao unatarajiwa kuwezesha binadamu kwenda Mars kufikia miaka ya 2030.

Rais Obama alitangaza mpango wake wa kupeleka binadamu Mars mwaka 2010.
Lakini mpango wa idara ya anga za juu ya Marekani Nasa wa kutimiza ndoto hiyo umekosolewa vikali, hasa na Bunge.
Kwenye makala aliyoandika, Rais Obama ameahidi kufanya kazi kwa pamoja na kampun za kibinafsi "kuunda mazingira mapya ambayo yanaweza kuhifadhi na kusafirisha wana anga".
"Tumeweka lengo lililo wazi kwenda katika sura nyingine ya historia ya Marekani katika anga za juu: nayo ni ya kutuma binadamu Mars miaka ya 2030 na kuwarejesha salama duniani. Katika hili kuna ndoto kuu kwamba wakati mmoja binadamu wataweza kwenda huko na kukaa kwa muda mrefu kiasi," Obama alisema kwenye makala katika tovuti ya kituo cha runinga cha CNN
Kampuni nyingi za kibinafsi, sana SpaceX, ambayo chombo chake cha Dragon hutumiwa kupeleka mizigo ISS, zimeweka wazi ndoto ya kupeleleza Mars.
Mwezi uliopita, Elon Musk, mwanzilishi wa SpaceX, alitangaza mpango wake wa kupeleka binadamu wakaishi Mars.
Baadhi walikosoa mpango huo wake wakisema ni ndoto isiyo na uhalisia wowote, lakini wengine wamemsifu kwa kutoa mpango wenye maelezo ya kina wenye lengo la kupeleka binadamu Mars.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment