Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga. |
Tanzania imeungana na nchini nyingine dunia katika kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo imesema licha ya kutofungamana na upande wowote, itaendelea kuwa na misimamo yake ikiwemo kuwa na uhuru, utu na ushirikiano wa mataifa mengine.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yanayofanyika tarehe 24 mwezi wa 10 kila mwaka.
Balozi Mahiga amesema kuwa watahakikisha kwamba somo la umoja wa mtaifa linaingizwa katika mitaala kuanzia shule za msingi ili vijana waweze kujua zaidi faida za kuwepo kwenye umoja huo kwa manufaa ya taifa.
Balozi Mahiga ameongeza kuwa serikali kupitia wizara yake imeweka mkakati wa kidiplomasia ambao utaiwezesha kukua kiuchumi kupitia umoja huo bila ya kukiuka misingi ambayo taifa imejiwekea.
No comments:
Post a Comment