Wednesday, 19 October 2016

Zitto Kabwe atoa neno hilli kuhusu ugomvi wa RC Arusha Mrisho Gambo na Godbless Lema.

Jana October  18 2016 kulifanyika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Burka nje kidogo ya jiji la Arusha, lakini shughuli hiyo ilisimama baada  mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kusimama kupinga maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Maelezo ya RC Gambo yalisema kwamba eneo la mradi ule limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala, maelezo ambayo mbunge Lema alikuwa akiyapinga na kudai yeye amehusika kutafuta ardhi na wafadhili, Lema alidai maelezo hayo yamejaa upotoshwaji na siasa ndani. Unaweza kuangalia video hii hapa chini.

Leo October 19 2016, mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa facebook ametoa ushauri kwa RC Gambo na Mbunge Lema, Zitto amesema…..…

"Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. 

"Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. 

"Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja. Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima."-Zitto Kabwe

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment