Monday 28 November 2016

Mshambuliaji Muivory Coast, Ya Thomas Renaldo atemwa na Klabu yake ya Azam FC.


Image result for Ya Thomas Renaldo azam fc
Azam FC imemuacha mshambuliaji Muivory Coast, Ya Thomas Renaldo iliyemsajili mwanzoni msimu baada ya kusajili washambuliaji watatu kutoka Ghana. 
Mapema mwezi huu, Azam FC iliwasaini washambuliaji Samuel Afful, Daniel Atta Agyei na Yahaya Mohammed wote kutoka Ghana.

Na ili kubaki na wachezajin saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni, Azam imewatema Waivory Coast wote, beki Serge Wawa, kiungo Kipre Michael Balou na mshambuliaji Renardo walioingia timu hiyo kwa wakati tofauti.



Balou alitangulia mwaka 2011 pamoja na pacha wake, Kipre Herman Tchetche ambaye mwanzoni mwa msimu alihamia Oman alikokwenda kujiunga na klabu ya Al Suwaiq, wakati Wawa alifuatia mwaka 2014, wakati Renaldo alisajiliwa Julai mwaka huu.  

Afful, Agyei na Mohammed wanafanya idadi ya wachezaji wa Ghana kufika wane, baada ya beki Daniel Amoah aliyesajiliwa Agosti.

Hao wanaungana na kiungo Jean Baptiste Mugiraneza kutoka Rwanda na Wazimbabwe wawli, winga Bruce Kangwa na mshambuliaji Francesco Zekumbawira kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.

Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki mbili hadi Desemba 3 mwaka huu, kitakapoanza mazoezi ya kwanza kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kombe la Shirikisho Afrika.


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE




                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment