Magoli ya Jordy Clasie na Ryan Bertrand yameitupa nje Arsenal kwenye kombe la EFL na kuipeleka Southampton hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye hajawahi kutwaa taji hilo katika miaka yake 20 aliyoishi London, alifanya mabadiliko ya wachezaji 10 kwenye kikosi cha Arsenal kilichoshinda 3-1 dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa Premier League Jumapili iliyopita.
Southampton ambao wameshinda mara moja katika michezo 23 waliyosafiri kuifata Arsena, walistahili ushindi na watacheza dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa kwenye uwanja wa St Mary January 9 mwaka ujao.
Vile vile Timu ya Manchester united wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa kufanikiwa kuifunga westham kwa magoli 4-1 magoli ya Man u yalifungwa na Ibrahimovic katika dakika ya 2 na 90 ,Martial 48, 62 huku goli la kufutia machozi la westham likifungwa na Fletcher
Nusu Fainali
Manchester United v Hull City
Southampton v Liverpool
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment