Monday 23 January 2017

Ifahamu tuzo nyingine aliyoshinda Bilionea Mohammed Dewji.

Image result for Mohammed Dewji
Bilionea kijana zaidi barani Afrika, Mtanzania Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Kiongozi Bora Afrika katika hafla iliyofanyika jijini Zurich nchini Uswiss.

Dewji maarufu kama Mo ameshinda tuzohiyo inayojulikana kwa jina la African Leadership Person of The Year ambayo hutolewa kwa wafanyabiashara au viongozi wanaofanya vizuri.


Mohammed Dewji.

Mo ameshinda tuzo hiyo ambayo ni heshima kubwa kwake kwa kuwa watu kadhaa maarufu walikuwa wakipewa nafasi ya kuitwaa.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MeTL Ltd, hivi karibuni aliweka dau la Sh bilioni 20 kutaka kununua hisa asilimia 51 katika klabu ya Simba.

Kabla amekuwa mdhamini na mfadhiri wa klabu hiyo akiwa msaada mkubwa wakati ikifika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuing’oa Zamalek.

No comments:

Post a Comment