Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho Jumanne
Waziri Mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayopitia Dodoma kuelekea Kigoma
Katika Uwanja wa Ndege Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wa serikali na chama wa mkoa wa Dodoma
Vikao vya Bunge vinaanza kesho baada ya wiki mbili za shughuli za kamati za kudumu za Bunge, na sasa tayari wabunge wamekwishawasili Dodoma kwa ajili ya vikao hivyo vitakavyodumu kwa takriban wiki 2
No comments:
Post a Comment