Monday, 20 February 2017

Alichokiona Profesa Jay katika gereza la Ukonga baada ya kwenda kumuona Mbunge Lijuakali.

Image result for Joseph Haule
January 11 2017 Mbunge wa Jimbo la Kilombero Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Peter Lijualikali alihukumiwa na Mahakama ya wilaya kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

February 19 2017 Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa J amekwenda kumtembelea gerezani Ukonga Dar es salaam na baada ya kutoka hapo akaandika yafuatayo.

‘Nimetoka gereza la Ukonga kumwona Mh. Lijualikali na Patron wa mkoa wa Morogoro kamanda Zinga na wapiga kura wangu watatu kutoka kata ya TINDIGA walifungwa miaka 30, wana afya njema na wanawasalimia sana ila wanalalamika tu hali sio nzuri kabisa kule ndani.. Mungu AWASAIDIE .

No comments:

Post a Comment