Saturday 30 April 2016

Kauli ya serikali kuhusu Uwekezaji Elimu ya Mtoto wa Kike.


 
Serikali ya awamu ya tano imesema inaendelea kuwekeza katika kutoa kipaumbele ya elimu kwa mtoto wa kike ili kusaidia kumuinua na kujikwamua katika maisha yake ya baadae.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya wasichana ya wama na kayama inayomilikiwa na mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete, waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi.Ummy Mwalimu amesema serikali inatambua mchango mkubwa ambao unatolewa na wadau mbalimbali wa elimu katika kumnyanyua mtoto wa kike kupata elimu ambayo ndio mkombozi mkubwa katika maisha yao.

Ummy Mwalimu amesema serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau ili kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa kwa kiwango cha juu na kufanikisha malengo ambayo serikali ya awamu ya tano imejipangia katika sekta ya elimu nchini.

Kwa upande wake balozi wa Japani nchini Hiroyuki Kubota ambao ndio wafadhili wa shule ya wama na kayama ,wamesema wataendelea kusaidia shule hiyo ili kuinua sekta ya elimu na pia kumsaidia mtoto wa kike.

No comments:

Post a Comment