Saturday 30 April 2016

Hii ndio Kauli ya Tume ya haki za binadamu na utawala kuhusu bunge kuoneshwa moja kwa moja(LIVE)

Bunge
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imesema kitendo cha bunge kuzuia kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge ni kuminya uhuru wa wananchi kupata habari.

Akizungumza wakati wa kutoa tuzo za Umahiri wa uandishi wa Habari kwa Mwaka 2015 , jaji Bahame Nyanduga amesema kumekuwepo na sheria ambazo zinasababisha kuminya uhuru wa vyombo vya habari , jamboa ambalo si sahihi kwa mustakabali wa taifa na kwa wananchi kwa ujumla.

Jaji Nyanduga amesema ni muhimu kwa wadau wa habari kukaa pamoja kutathmini na kujadiliana namna ambavyo wanaweza kupaza sauti kwa pamoja katika kupigania uhuru wa habari .

Katika utoaji wa tuzo hizo, Channel ten ni miongoni mwa vituo vya televisheni ambavyo waandishi wake wamepata tuzo hizo ambapo mwandishi wake wa habari Esther Zelamula amepata tuzo ya mazingira,Cassius Mdami amepata tuzo ya uchumi na biashara pamoja na Khamis Suileman amepata tuzo ya uchunguzi , wakati Bi Rose Haji amepata tuzo ya mafanikio.

No comments:

Post a Comment