Saturday 30 April 2016

Maamuzi ya Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya TFF kuhusu Kocha Stewart na wachezaji 15 haya hapa


Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya TFF kilichopangwa kufanyika hapo kesho Mei Mosi 2016, kimeahirishwa hadi Jumanne Mei 3, mwaka huu.

Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kwamba baadhi ya wajumbe wamepata udhuru hivyo wangeshindwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika mjini Dar es Salaam kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.

Kikao hicho kinatarajiwa kujadili kesi za wachezaji John Bocco (Azam FC), Shomari Kapombe (Azam FC), Aishi Manula (Azam FC), Amissi Tambwe (Yanga SC), Donald Ngoma (Yanga SC), Paulo Jinga (JKT Rwamkoma FC) na Kipre Tchetche (Azam FC).
Wengine ni Abel Katunda (Transit Camp), Zephlyn Laurian (JKT Rwamkoma FC), Idrisa Mohamed (JKT Rwamkoma), Mganaga Kitambi (Daktari wa Coastal Union), Herry Chibakasa (Friends Rangers), Ismail Nkulo (Polisi Dodoma), Said Juma (Polisi Dodoma), Idd Selaman (Polisi Dodoma), Edward Amos (Polisi Dodoma) na kocha Stewart Hall (Azam FC).

No comments:

Post a Comment