Saturday 30 April 2016

Makonda kila mtaa utakaoshinda kwa Usafi utapata shiling milion 50.

OTH_5714
Mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda amezindua kampeni ya Usafi katika jiji la dar es salaam litakaloendeshwa na Viongozi wa serikali za mitaa na wajumbe wao huku kila mtaa utakaoshinda kwa Usafi utapata shiling milion 50.



Aidha katika mkutano huo uliokuwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za kinondoni,temeke na Ilala Mkuu huyo alitangaza kufanyika Uchunguzi kwa viongozi wote wa jiji na manispaa ambao ni watumishi huku pia wakimiliki kampuni za usafi na ikibainika watachukuliwa hatua kutokana na kanuni za utumishi wa umma.

Makonda pia ametangaza kila jumamosi ya mwisho wa wiki kufanyika zoezi la usafi na biashara zote zitafunguliwa baada ya saa tatu na atakayekaidi atachukuliwa hatua huku askari wa usalama barabarani wakipewa agizo la kukamata daladala zote kuanzia jumatatu zisizokuwa na vifaa vya kuhifadhia uchafu.

Mkuu wa wilaya ya kinondoni Ali salum hapi katika kuwashughulikia watumishi wasiowajibika aliwasimamisha kazi mara moja na kumtaka mkurugenzi wa manispaa ya ilala kuchukua hatua nyingine kabla ya saa sita kesho baada ya kubainika kutoshiriki na kusimamia zoezi hilo la Usafi ambalo kilele chake kilifikia katika viwanja vya leaders club.

Vingozi wengine waliokuwapo walilisitiza wananchi kuzingatia Usafi na kutangaza kusimamia sheria kwa wananchi watakaoshindwa kushiriki au kuweka mazingira yako katika Usafi.

No comments:

Post a Comment