Saturday 30 April 2016

Sheria na taratibu za kazi wanachuo watahadhalishwa Tazama hapa

jairo
Vijana waliopo vyuoni wametahadharishwa kuhusu athari za kutozingatia kikamilifu maadili, sheria na taratibu za kazi wakati wote na mahali popote mara watakapofika kwenye vituo vya kazi, na kwamba wanawajibika kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Tahadhari hiyo imetolewa katika maadhimisho ya siku ya CAREER, katika chuo cha kodi nchini, siku ambayo hutoa fursa kwa wanafunzi, wahadhiri na waajiri kutoka taasisi mbalimbali kukutana kwa lengo la wanafunzi kuonyesha waliyojifunza kwa vitendo, ambapo Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala wa mamlaka ya mapato Tanzania, Victor Kimaro, amesema vijana wengi wanaponzwa na tamaa ya kupata mali mapema na hivyo kukiuka maadili ya kazi.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa chuo cha kodi kuadhimisha CAREER day, mkuu wa chuo hicho Profesa Isaya Jairo, amesema maendeleo ya taifa lolote yanategemea ujuzi wa asili, ujuzi wa kujifunza na ubunifu, changamoto ni kuhakikisha chuo cha kodi kinazalisha wasomi ambao wataweza kukabiliana na ushindani duniani.

Kwa upande wa wanafunzi wa chuo cha kodi wameelezea matumaini yao kwa siku hiyo ya CAREER, na kusema inawajenga katika uhalisia wa utendaji wa taaluma yao.

No comments:

Post a Comment