Kero ya muda mrefu ya upungufu wa madawati na uchakavu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Narakauo iliyoko katika kijiji cha Narakauo kata ya Loibosireti wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, inaweza kupungua au kuisha kabisa baada ya Diwani wa kata hiyo Ezekiel Lesenga na marafiki zake kutoa jumla ya madawati mia moja, mifuko tisini na tatu ya saruji na fedha taslim vitakayotumika kukarabati madarasa.
wanafunzi hao ambao viti yao vilikuwa ni vipande vya matofali,vibakuli na magoti yao kugeuka kuwa meza lakini kama hiyo haitoshi madarasa nayo ni vumbi tupu hapa suala la usafi likiwa ni ndoto Na hata wakati mwingine kuchukia masomo,diwani wa kata hiyo Ezekiel Lesenga almaarufu Maridadi kwa kushirikiana na wenzake wanawanusuru watoto hawa na Hali hiyo kwa kutoa madawati 100 na kufanya Harambee ya wazazi kwa ajili ya ukarabati wa madarasa shuleni hapo.
Ni watoto wa shule ya msingi Narakauo wakionekena wenye furaha na matumaini mapya ya kupata elimu ya msingi baada ya kuwa na uhakika wa kukaa kwenye madawati na kukarabatiwa madarasa yao Masaada unaenda na sambamba na kukabidhiwa vifaa vya michezo
No comments:
Post a Comment