Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kabla ya Uteuzi huo Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
Bw. Clifford Tandari anachukua nafasi ya Dkt. John Ndunguru ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Clifford Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Mei, 2017
No comments:
Post a Comment