Tuesday, 27 June 2017

Masaa manne ya Edward Lowassa ndani ya Jeshi la polisi hii leo.


Image result for edward lowassa kituo cha polisi
Mjumbe wa kamati kuu na mgombea urais mwaka 2015 ndugu Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya Polisi saa nne kama alivyoambiwa na DCI.

Lowassa alikuwa amefuatana na Magari manne ya kwake pamoja na magari mawili ya polisi wenye Silaha.

Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji. Aliwasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.

Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.

Kwa lolote litakalotokea tutazidi kujuzana.

Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.

Mahojiano Kati ya Mh Lowasa na DCI yamechukua masaa 4. Atatakiwa kuripoti tena siku ya Alhamisi,saa 6 mchana.

Sababu za kuhojiwa kwake ni juu ya kauli alizozitoa wakati wa futari alipokuwa akiongea na waumini wa dini ya kiislam.

Hatma ya alichoitiwa itajulikana siku ya Alhamisi

No comments:

Post a Comment