Wednesday 19 July 2017

Kocha wa Yanga Lwandamina atoa neno kwa Simba.


Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, raia wa Zambia, ameonekana kuwa bize sana kukiandaa kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri msimu ujao huku akisema hana muda wa kuwafuatilia wapinzani wake wa msimu ujao, wakiwemo Simba SC.

Mzambia huyo aliyejiunga na Yanga Novemba, mwaka jana, amesema wala hafahamu chochote kuhusiana na wanachokifanya Simba kwa sasa kutokana na kwamba hana muda wa kuzifuatilia timu nyingine zaidi ya ile anayoifundisha.

Wakati Lwandamina akiyasema hayo, timu hizo zinatarajiwa kukutana Agosti 23, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kuanza kwa msimu mpya.

“Nafanya kazi Yanga, hivyo siwezi kuzifuatilia timu nyingine nikaiacha timu yangu, nimeajiriwa kwa ajili ya Yanga na si timu nyingine, najua maandalizi ninayowapa vijana wangu ni bora na yatatupa matokeo mazuri.


“Siwezi kuizungumzia Simba kwa sasa inavyojipanga kwa kufanya usajili kutokana na kwamba sifuatilii chochote kutoka kwao,” alisema Lwandamina.

No comments:

Post a Comment