Thursday 20 July 2017

Mahakama yatoa maamuzi kuhusu kesi ya Viongozi wa Simba.

Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba, Rais  Evans Aveva na Makamu Rais, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imetajwa leo Julai 20 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Aveva peke yake aliweza kufika mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na taarifa za nje ya mahakama zimeeleza kwamba Kaburu akishindwa kufika mahakamani kutokana na kudaiwa kuwa ni mgonjwa.

Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande baada ya kesi yao kuahirishwa na sasa watarejeshwa mahakamani hapo Julai 31, mwaka huu.

Kabla ya kesi hiyo kutajwa wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.


Awali kulikuwa na taarifa huenda leo wangepata ahueni na kuachiwa kwa dhamana.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE




                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment