Simba imeendelea na mazoezi yake kama kawaida ikiwa chini ya nahodha mpya, Method Mwanjale.
Mwanjale ndiye nahodha aliyechukua nafasi ya Jonas Mkude aliyekuwa nahodha msimu uliopita.
Kikosi cha Simba kipo katika maandalizi ya msimu katika kambi yake ya nchini Afrika Kusini.
Mkude ni kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakifanya mazoezi kwa juhudi kubwa kuhakikisha wanakuwa imara kwa ajili ya msimu ujao.
Kubadilishwa unahodha kwa Mkude, kumezua gumzo kubwa hasa mitandaoni lakini inaonekana wachezaji wa Simba wamelichukulia kawaida na kuendelea na majukumu yao.
No comments:
Post a Comment