Manchester United imeonyesha imepania kupindua kabati baada ya kukubaliana na Everton kuhusiana na uhamisho wa Romelu Lukaku kwa pauni milioni 75.
Chelsea ndiyo walionekana na matumaini ya kumnasa Lukaku lakini kocha wake Antonio Conte anaonekana kuchanganyikiwa huku Jose Mourinho akionyesha kweli ni Mafia.
Imeelezwa Lukaku anatarajia kufanya vipimo vya afya na sasa yuko Los Angeles, Marekani akiwa na swahiba wake Paul Pogba, ambaye ni kiungo nyota wa Man United.
Pogba hajaonekana katika mazoezi ya Everton inayojiandaa kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki Julai 13.
Dalili zote zinaonekana atapishana na safari hiyo kwa kuwa Mourinho yuko siriaz kweli kuhakikisha anatua United na kuwa shetani mpya.
No comments:
Post a Comment