Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi amefanya mauaji leo uwanja wa Taifa baada ya kufunga jumla ya magoli manne kati ya magoli saba ya Simba dhidi ya klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18.
Kikosi cha Simba ambacho kilikuwa chini ya Kocha Mkuu wake, Joseph Omog kilianza kwa mashambulizi makali ndani ya dakika za mwanzo za mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na kumpelekea Emmanuel Okwi kuweza kupata bao la kwanza ndani ya dakika 18 ya mchezo.
Simba waliendeleza mashambulizi na nia ya kupata ushindi wa haraka dhidi ya Ruvu Shooting na ilipofika dakika ya 22 Emmanuel Okwi tena aliweza kuwainua mashabiki wa Simba kwa kupachika goli la pili ndani ya dakika ya 22 ya mchezo.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa Ruvu Shooting kwa kukubali mashambulizi ya haraka haraka kutoka kwa Simba jambo ambalo liweza kutoa nafasi nyingine tena kwa mshambuliaji huyo wa Kimataifa raia wa Uganda kupachika goli la tatu katika dakika 35 ya mchezo huku Ruvu Shooting wakiwa hawana bao hata moja.
Klabu ya Simba ilizidi kufanya mashambulizi makali dhidi ya Ruvu Shooting na katika dakika ya 42 Shiza Kichuya aliwainua tena mashabiki wa Simba kwa kupachika goli la nne huku Juma Liuzio naye aliweza kuipatia Simba goli la tano katika dakika ya 45 ya mchezo.
Mpaka wanakwenda mapumzikoni Simba walikuwa wanaongoza kwa bao 5 kwa 0 dhidi ya Ruvu Shooting, kipindi cha pili kilipoanza Simba waliendeleza mashambulizi yao kama kawaida wakiwa na lengo la kutafuta zaidi magoli katika dakika ya 53 Okwi aliweza kuwapa furaha mashabiki wa Simba kwa kupachika goli la sita katika mchezo huku kwake yeye akiwa anatimiza goli la nne.
Wachezaji wa Simba hawakuridhika na magoli hayo waliendeleza mashambulizi na ndani ya dakika 80 ya mchezo Erasto Nyoni aliweza kuipatia Simba goli la saba, mpaka mpira unakwisha Simba walitoka kifua mbele kwa bao 7- dhidi ya Ruvu Shooting.
Kwa hatua hiyo Emmanuel Okwi ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye magoli mengi katika ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 kwa kuweza kuwa na jumla ya magoli manne.
SIMBA SC
1. Aishi Manula-28
2. Ally Shomary-21
3. Erasto Nyoni-18
4. Method Mwanjale-17
5. Salum Mbonde-2
6. James Kotei-3
7. Shiza Kichuya-25
8. Mzamiru Yassin-19
9. Juma Liuzio-10
10. Emmanuel Okwi-7
11. Haruna Niyonzima-8
SUB
1. Emmanuel Mseja-30
2. Jonas Mkudeh-20
3. Mohamed Ibrahim-4
4. Said Ndemla-13
5. Laudit Mavugo-11
6. Juuko Murshid-6
7. Mohamed Hussein-15
Kocha...
MARIUS OMOG
RUVU SHOOTING.
1. Bidii Hussein-18
2. Said Imani Madega-19
3. Yusuph Innocent-2
4. Shaibu Nayopa-26
5. Mangasin Mangasin-6
6. Baraka Mtuwi-15
7. Chande Magoja-21
8. Shaban Msaja-4
9. Juma Said-9
10. Jamal Mtegeta-10
11. Khamis Mussa-22
Subs.
1. Abdallah Rashid-1
2. George Wawa-12
3. Mau Ally-23
4. Frank Msese-16
5. Kassim Dabi-24
6. William Patrick-27
7. Said Dilunga-25
Kocha..
ABDUL MUTIK HAJI
Kick Off-16:00
Venue: Uhuru Stadium.
1. Aishi Manula-28
2. Ally Shomary-21
3. Erasto Nyoni-18
4. Method Mwanjale-17
5. Salum Mbonde-2
6. James Kotei-3
7. Shiza Kichuya-25
8. Mzamiru Yassin-19
9. Juma Liuzio-10
10. Emmanuel Okwi-7
11. Haruna Niyonzima-8
SUB
1. Emmanuel Mseja-30
2. Jonas Mkudeh-20
3. Mohamed Ibrahim-4
4. Said Ndemla-13
5. Laudit Mavugo-11
6. Juuko Murshid-6
7. Mohamed Hussein-15
Kocha...
MARIUS OMOG
RUVU SHOOTING.
1. Bidii Hussein-18
2. Said Imani Madega-19
3. Yusuph Innocent-2
4. Shaibu Nayopa-26
5. Mangasin Mangasin-6
6. Baraka Mtuwi-15
7. Chande Magoja-21
8. Shaban Msaja-4
9. Juma Said-9
10. Jamal Mtegeta-10
11. Khamis Mussa-22
Subs.
1. Abdallah Rashid-1
2. George Wawa-12
3. Mau Ally-23
4. Frank Msese-16
5. Kassim Dabi-24
6. William Patrick-27
7. Said Dilunga-25
Kocha..
ABDUL MUTIK HAJI
Kick Off-16:00
Venue: Uhuru Stadium.
No comments:
Post a Comment