Mfanyabiashara na aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amekutwa na kesi ya kujibu katika shitaka la analotuhumiwa kutumia madawa ya kulevya.
Kesi hiyo iliyokuwa na mvutano takribani siku tatu hasa kuhusu mkojo wa nani ulipimwa na mkemia kubaini Manji anatumia madawa ya kulevya.
Akitoa maamuzi hayo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa ana haki ya kujitetea kutokana na mkojo wake kukutwa na dawa aina ya Morphine ambayo zao lake ni Heroin
Aidha alieleza kuwa mshtakiwa huyo ana haki ya kujitetea kama wakili wa serikali, Timon Vitalis alivyopeleka mshahidi waake wa kesi hiyo mahakamni hapo.
Kwa upande wake, wakili upande wa utetezi, Hudson Ndisyepo aliiambia mahakama hiyo kuwa mteja wake ataanza kuleta mashahidi wake 15 ili kesi hiyo isikilizwe kwa mfululizo Agosti 30 na 31 mwaka huu.
Kesi hiyo ilikuwa imekuja leo kwa ajili ya shauri hilo kusikilizwa kama endapo mtuhumiwa ana kesi ya kujibu ama la, kuhusiana na kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment