Ile aina ya uchezaji wa beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambayo amekuwa akionyesha uwanjani tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, imewashitua vilivyo viongozi wa Simba, lakini Omog amesema anamfahamu.
Tangu Ninja ajiunge na Yanga amekuwa gumzo kubwa kwa mashabiki wa soka hapa nchini kutokana na aina ya uchezaji ambayo imesababisha baadhi ya washambuliaji anaokutana nao uwanjani wamuogope wakihofia kuumizwa.
Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Simba wameingiwa na hofu kuwa mchezaji huyo anaweza kusababisha baadhi ya wachezaji wao ambao husumbuliwa na majeruhi mara kwa mara kuumia, hivyo kuwafanya washindwe kuitumikia timu hiyo katika baadhi ya mechi zao za ligi kuu msimu ujao.
“Ni matumaini yetu kuwa taarifa hizo atazifanyia kazi ili wachezaji wetu waweze kuwa makini pindi watakapokutana na mchezaji huyo uwanjani katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
“Aina ya uchezaji wa Ninja ni hatari sana kwani anaweza kutuumiza wachezaji wetu na tukawakosa kwa muda mrefu katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa Omog kuhusiana na suala hilo alisema kuwa: “Ni kweli kabisa taarifa za Ninja nimezipata lakini pia nimeshamuona akicheza kwa hiyo ninajua jinsi gani ya kukabiliana naye.”
No comments:
Post a Comment