Mshambuliaji Wayne Rooney wa Everton amefunga bao lake la 200 katika Ligi Kuu England wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Man City.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho alikuwa uwanjani hapo akishuhudia mechi hiyo kwenye Uwanja wa Etihad.
Everton wanaodhaminiwa na SportPesa waliokuwa ugenini ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 36 kupitia Rooney aliyeunganisha pasi ya chinichini.
Pia Man City ikapata pigo baada ya Kyle Walker, beki wa kulia huyo kulambwa kadi ya pili ya njano ndani ya dakika mbili na kuzaa nyekundu.
Pamoja na Everton kuwa na mtu mmoja zaidi lakini ilishindwa kutawala mchezo na kuwapa City nafasi kubwa ya kucheza hadi waliposawazisha katika dakika ya 82 kupitia Raheem Sterling baada ya beki wa Everton.
Dakika ya 88, Morgan Schneiderlin kulambwa kadi ya pili ya njano na kuandika nyekundu. Hata hivyo, picha za marudio zilionyesha hakumgusa Kun Aguero badala yake aligusa mpira.
No comments:
Post a Comment