Mwenyekiti wa (CUF) anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ni kama ameendelea kupoteza heshima yake katika jamii kutokana na maoni mbalimbali ya watu kwa jinsi wanavyomuona sasa.
Jana Profesa Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo yanaendelea ndani ya CUF hali hiyo ni kama ilijidhirisha Profesa huyo kuonekana anapoteza ile heshima aliyokuwa amejijengea awali katika jamii kwa muda mrefu kufuatia michango mbalimbali ya watu kwenye mitandao ya jamii ambao walionekana wazi kumnyooshea kidole na kumwita msaliti huku wengine wakimbeza kuwa hana sifa tena za kuendelea kuwa profesa, hali ambayo inaonyesha wazi kuwa watu hao hawana imani naye tena kwa kila anachofanya hata kama kinaweza kuwa na ukweli ndani yake.
Baadhi ya maoni ya watu katika mitandao ya kijamii. |
Mbali na michango hiyo ya watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii tarehe 24 April 2017 Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF Mh. Abdallah Mtolea alifunguka na kusema kuwa alikuwa anamuheshimu sana Profesa Lipumba kiasi kwamba kuna wakati alikuwa haitaji kuongea jambo lolote kuhofia kukosea heshima kiongozi huyo lakini kwa mambo aliyoyafanya ndani ya Chama chao alifika hatua ya kumshusha na kudai kuwa Profesa huyo hivi sasa amepoteza heshima ambayo alikuwa nayo awali katika jamii.
"Mimi Lipumba ni kama kaka yangu kwa jinsi nilivyokuwa namuheshimu, lakini pia alikuwa kiongozi wangu bado namheshimu ila kwa kitendo kilichofanyika pale VINA nimeishusha heshima yangu kwake kwa kiasi kikubwa sana na niseme tu amekuwa mtu wa ajabu sana, elimu yake yote na heshima aliyonayo amekuja kuiharibu kwa mambo ya ajabu kama anayoyafanya" alisisitiza Mh. Mtolea
Profesa Ibrahim Lipumba ni mchumi wa kimataifa ambaye alijizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na kuheshimika sana kutokana na michango yake kwa taifa katika masuala ya kiuchumi, lakini kisiasa pia aliheshimika sana miongoni mwa wafuasi wake kwa mitazamo yake na misimamo yake thabiti ambayo ilionyesha kutoyumba, mwaka 2015 kiongozi huyu aliamua kujiuzulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa CUF Taifa.
Nini maoni yako katika hili?
No comments:
Post a Comment