Friday, 18 August 2017

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine.

Related image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.


Taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaam inasema Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, kuchukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.

Wakati huo huo Rais Magufuli amewateua Prof. Abdulkarim Khamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya kuhifadhi mafuta (TIPER), ambaye kabla alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Jiologia Tanzania, na Prof. Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania LTD.

Prof. Buchweshaija alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).

No comments:

Post a Comment