Kesi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo imeendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo upande wa mashtaka umeieleza mahakama hiyo kwamba umekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu hivyo uliiiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu.
Aidha hakimu aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha ripoti hiyo ya uchunguzi akisema kwamba watuhumiwa wako rumande hivyo si bora kesi hiyo kuahirishwa kila mara.
No comments:
Post a Comment