Baaada ya kimya cha muda mrefu Askofu Mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima,
Mchungaji Josephat Gwajima ameibuka na kutangaza kuleta ndege aina ya
'Jet' Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wake.
Mchungaji Gwajima ambaye hivi sasa yupo mjini Birmingham, Alabama nchini Marekani kwa shughuli zake za injili na mikutano mbalimbali ameahidi ataleta ndege aina ya 'Jet'
"Muda si mrefu nitaleta Tanzania ndege hii 'Jet' kwa lengo la kukuza falme ya Mungu" alisema Gwajima
"Nimepata Umeme Megawati 250
kutoka Ujerumani kwa ajili ya Taifa letu katika juhudi za kuunga mkono
Tanzania ya Viwanda. Nilimtuma Engineer Mkuu wa Ufufuo na Uzima Duniani
Eng.Yeconia Bihagaze huko Ujerumani kufanya ufuatiliaji, Umeme huu ni
kwa ajili ya Watanzania wote na ujenzi wa uchumi imara wa Tanzania ya
Viwanda" alisema Mchungaji Gwajima
VIDEO
Hata hivyo mchungaji Gwajima aliwahi kuahidi pia ataleta treni la kisasa linalotumia Umeme Tanzania.
No comments:
Post a Comment