Saturday, 17 March 2018

Hii ndio teknolojia mpya itakayotumika katika michuano ya Kombe la Dunia

Image result for rais wa fifa
Teknolojia ya Video Assistant Referees (VAR), imethibitishwa rasmi kutumika kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia.


Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amethibisha hilo leo.

Majaribio ya teknolojia hiyo ya VAR yalifanyika katika nchi za Germany na Italy katika msimu huu.

Infantino amesema inabidi mpira wa soka uishi kuendana na wakati hivyo amefikia hatua hiyo ili kuwasaidia Waamuzi kutoka maamuzi sahihi Uwanjani.

"Tunahitaji kuishi kuendana na wakati, tulihitaji kuwapa Waamuzi vifaa ambavyo vitawasaidia kutoa maamuzi sahihi Uwanjani" alisema.


No comments:

Post a Comment